SHULE YA SIZAKI YEPEWA UFADHILI WA BWENI NA UBALOZI WA JAPANI

July 20, 2017

Shule ya Sizaki ilipata Ufadhili wa Ubalozi wa Japan na kukabidhiwa bweni la wasichana mwaka 2016. Hii ni baada ya Mtandao wa Madeni na Maendeleo Tanzania kwa kushirikiana na taasisi ya FAOUNDATION HELP ya mjini BUNDA Walipofanya tathmini ya hali ya elimu katika shule za sekondari Wilaya ya Bunda na kubaini changamoto inayowakumba wanafunzi hasa watoto wa kike kwa kutembea umbali mrefu mpaka kufika shule. Mrejesho wa tathmini hiyo ulifanyika kwa kuwashirikisha wadau wa elimu wakiwemo madiwani ambapo Mh. Stephen Wasira (aliyekuwa Mmbunge) alilifanyia kazi na ufadhili huu ulipatikana.

Mabweni mawili yalijengwa. Bweni moja lilijengwa kwa ufadhili wa Japani na moja lilijengwa kwa michango ya wazazi kwa kushirikiana na Serikali ambalo halijakamika mpaka sasa na linahitaji msaada wa kulikamilisha. Kila bweni lina vitanda 48 kwa yote mawili ni sawa na vitanda 96, hivyo Wasichana 96 wanaweza kulala shuleni. Kwa sasa Wasichana 71 ndio wanaolala bwenini kwa sasa

Maandalizi ya bweni la wasichana mwaka 2013 Hiki kilikuwa ni chumba cha Darasa ( Jiko likiwemo na Wanafunzi wakijisomea pembeni, na vitanda ndani)

Maandalizi ya bweni la wasichana mwaka 2013 Hiki kilikuwa ni chumba cha Darasa (Jiko likiwemo naWanafunzi wakijisomea pembeni, na vitanda ndani)

Katokana na  mafanikio haya shule imepokea wanafunzi kutoka kata za jirani za Bunda mjini, Musoma, Magu na Mwanza. Tunapenda kuishukuru serikali kwa kuboresha miundo mbinu mbalimbali katika shule hii ikiwemo: kuongeza vitabu vya kiada hasa katika Sayansi,  kuongeza Madawa na  kuboresha miundombinu ya Umeme

Pamoja na mafanikio hayo bado kunachangamoto za; uhaba wa  nyumba za Walimu, uhaba wa vifaa vya maabara, uhaba wa waalimu hasa wa masomo ya sayansi na ubovu wa miundombinu ya kufika shuke mfano madaraja, uchakavu wa barabara hasa wakati wa mvua

Muonekano wa jesho la Bweni lililofadhilia katika shule ya sekondari Sizaki

Muonekano wa jesho la Bweni lililofadhilia katika shule ya sekondari Sizaki

Muonekano wa ndani ya bweni

Muonekano wa ndani ya bweni

Picture5

Uonekano wa nje na ndani wa Jengo la Choo, Bafu, Tanki la maji na sehemu ya Kufualia

Uonekano wa nje na ndani wa Jengo la Choo, Bafu, Tanki la maji na sehemu ya Kufualia