Hali ya Elimu na Afya na changamoto zake Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma
Utafiti na ufuatiliaji wa fedha zinazotolewa na serikali katika sekta ya elimu na afya ni muhimu sana ili kujua kama zinafanya kazi iliyokusudiwa. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bi Hanji Yusufu Godgod alipokuwa akifungua mkutano na wadau wa sekta ya elimu na afya, Mkutano uliolenga kutoa mrejesho wa utafiti uliofanywa na asasi ya kiraia ya KIUNGONET ikishirikiana na taasisi ya Mtandao wa Madeni na Maendelea Tanzania(TCDD).
Utafiti ulikuwa unaangalia hali ya elimu na afya kwa mwaka 2012-2014 katika halmashauri ya wilaya ya Kigoma na ulifanywa katika shule kumi za sekondari ambazo ni Mkuti, Mkongoro, Kalinzi, Mwandiga, Nyarubanda, Luiche, Zashe, Bugamba, Bitale na Matiazo na vituo vitano vya afya ambavyo Mwandiga, Bitale, Pamila na Kagunga