Halmashauri ya manispaa ya Iringa yadhamiria kuboresha Elimu

Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imedhamiria kuboresha miundombinu kwenye shule za sekondari. Akizungumza kwenye kikao cha mrejesho kuhusu tathimini ya hali ya elimu uliofanywa na Wise Utilization for Natural Resource Sustainability (WURNS) ambaye ni mwanachama wa Matandao wa Madeni na Maendeleo Tanzania (TCDD) tarehe 9, Februari 2021 katika manispaa hiyo. Tathini hii ilijumuisha shule kumi kutoka katika kata kumi za manispaa ya Iringa. Kata hizo ni pamoja na Mlandege, Kihesa, Kwakilosa, Miyomboni, Mtwivila, Ipogolo, Kleruu, Mlamke, Mkwawa na Nduli.   Mstahiki Meya wa manispaa Mh Ibrahim Ngwada mesema serikali imejipanga kukarabati miundombinu  ikiwa ni pamoja na kujenga mabweni katika shule ya sekondari kata ya Nduli ambapo ilibainika kuwa na changamoto ya umbali kwa wananfunzi hususani watoto wa kike  waliopo kwenye hatari kubwa ya kukatisha masomo yao. Kikao hiki kilijumuisha wadau wa elimu kutoka ngazi ya manispaa ikiwemo madiwani wa kata zote, afisa elimu manispaa, waalimu wa shule za sekondari zilizofanyiwa tathmini, wawakilishi wa wazazi na wawakilishi wa wanafunzi. Pamoja na makubaliano yaliyofikiwa kikao kilibainisha kuwa miradi hasa iliyoanzishwa miaka mitatu iliyopita itapewa kipaumbele kabla ya kuanzisha miradi mipya. Miundominu iliyokusudiwa kuboreshwa ni pamoja na kumalizia miradi ya majengo ya maabara, maktaba na kuongeza vyumba vya madarasa pamoja na vyoo kwenye shule zilizo na uhaba. Mstahiki Meya amesema kuwa hawataanzisha miradi mipya mpaka iliyokuwa imeanzishwa ikamilike.