Deni La Taifa ni Himilivu
Akisoma hotuba ya Hali ya Uchumi kwa mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2021 nchini Tanzania, Waziri wa Fedha na Mipango Mh Dr. Mwigulu Nchemba ameyasema haya leo Bungeni. Mheshimiwa waziri amesema hadi kufikia April 2021 Deni la Taifa ni TSh 60.9 trilioni ambapo Deni la nje ni ni Tsh 43.7 trilioni na Deni la ndani ni TSh 17.3 trilioni. Amesema deni hili linatokana na kupokelewa kwa fedha za mikopo kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo. Kwa mujibu wa taarifa ya tathimini ya uhimilivu wa Deni la Taifa ya mwaka 2020, Deni la Taifa ni himilivu katika kipindi cha muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu kwa kuzingatia ukomo wa viashiria vyote vilivyokubalika kimataifa.