TCDD Yafanya semina kwa AZAKI jijini Dodoma kuhusu Deni la Taifa

Mtandao wa Madeni na Maendeleo Tanzania (TCDD) umefanya mafunzo kwa Asasi za kiraia leo tarehe 13.5.2024 Jijini Dodoma. Mafunzo hayo yalihusu mwenendo wa deni la Taifa la Tanzania, jukumu na wajibu wa Asasi za kiraia kuhusu kuishauri serikali juu ya ukopaji wa uwajibikaji.
Akifungua mafunzo hayo mkurugenzi mtendaji wa TCDD Bwana Hebron Mwakagenda amezikumbusha asasi za kiraia kuwa zina wajibu mkubwa kufuatilia mwenendo wa deni la Taifa na kuishauri serikali namma bora ya ukopaji, matumizi na ulipaji wa deni husika.
Katika kipindi cha mwaka 2022/2023 deni la taifa limeongezeka kwa asilimia 15% na kufikia Trilioni 82.25 kutoka mwaka 2021/2022 huku deni hilo likitajwa bado kuwa ni himilivu kwa mujibu wa Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali nchini Charles Kichere wakati uwasilishwaji wa Ripoti ya CAG na ripoti ya TAKUKURU kwa mwaka 2022/2023 kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan Ikulu ya Chamwino Dodoma.“Hadi kufikia tarehe 30 Juni 2023 deni la serikali lilikuwa Trilioni 82.25 sawa na ongezeko la asilimia 15 kutoka mwaka 2021/2022 na deni hili bado ni himilivu” – CAG Charles Kichere.
Kwa kuzingatia ongezeko hili la deni la Taifa ni wajibu wa Asasi za kiraia kuisimamia serikali kuitaka hela zote zinazokopwa zielekezwe kwenye miradi husika.

Leave a Reply