Tanzania Yaiomba EXIM Bank China isaidie pesa ujenzi wa SGR
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amefanya mkutano kwa njia ya mtandao kutoka Jijini Dodoma na Rais wa China Exim Bank, Ren Shengiun, ambapo wamejadili kuhusu ushirikiano kati ya Serikali na Benki hiyo ikiwemo upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo Nchini.
Katika mkutano huo pamoja na mambo mengine, DKT. Nchemba, ameiomba Benki hiyo kusaidia upatikanaji wa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) ambao ni miongoni mwa miradi ya kipaumbele ya Nchi kwa sasa.
Kwa upande wa Tanzania Mkutano huo umehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Amina Khamis Shaaban, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje wa Wizara hiyo, Rished Bade na Kamishna Msaidizi wa Usimamizi wa Madeni, Tiba Kisonga na Maafisa wengine wa Wizara.
#MillardAyoUPDATES