Tumelipa Tril.8.48 Deni la Serikali

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amesema hadi kufikia Aprili 2024, Wizara hiyo imelipa kwa wakati notisi za madai ya deni la Serikali lililoiva jumla ya shilingi trilioni 8.48, sawa na ufanisi wa asilimia 81 ya lengo la mwaka ambapo kati ya kiasi hicho deni la ndani ni shilingi trilioni 4.63, ikijumuisha riba shilingi trilioni 1.98 na mtaji shilingi trilioni 2.65 na deni la nje ni shilingi trilioni 3.83, ikijumuisha riba shilingi trilioni 1.34 na mtaji shilingi trilioni 2.49.

Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mwaka 2024/2025, Bungeni Jijini Dodoma leo June 04,2024, Mwigulu amesema “Kupitia kupitia Fungu 001, Bunge lako Tukufu liliidhinisha jumla ya shilingi trilioni 10.48 kwa ajili ya kuhudumia deni la Serikali pindi linapoiva”

Leave a Reply